By:Robert Mutasi

Kampuni ya Safaricom imezindua kampeni mpya ya kitaifa ya “Pata More”, inayowalenga wateja wake kwa kuwapa data zaidi, ofa za biashara na huduma nyingine zenye thamani kubwa zaidi kwa gharama ile ile.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Barabara ya Kangundo jijini Nairobi, Afisa Mkuu wa Wateja wa Safaricom, Fawzia Ali-Kimanthi, alisema kampeni hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 ya kampuni na ni njia ya kuwashukuru wateja kwa uaminifu wao katika kipindi hicho.
Kupitia kampeni hiyo, wateja watanufaika na Pata More Data, huduma za Pochi la Biashara, Home Fibre, pamoja na mikopo ya simu janja. Aidha, vifurushi vya siku, wiki na mwezi sasa vitakuwa na kiwango kikubwa zaidi cha data ili kuwapa wateja matumizi bora zaidi.
Uzinduzi huo umejiri wakati wanahisa wa Safaricom walipoidhinisha mgao wa rekodi wa shilingi bilioni 80.13, sawa na shilingi mbili kwa kila hisa, katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kampuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom, Peter Ndegwa, alisema kampuni itaendelea kuwekeza katika ubunifu na teknolojia ili kuwapa wateja huduma bora zaidi, huku msafara wa kampeni ya Pata More ukitarajiwa kufika katika kaunti mbalimbali nchini.
Wateja wanaotaka kunufaika na ofa hizo wanaweza kuzipata kwa kupiga *544# kwenye simu zao.
