Share this to

Idara ya Usalama katika Kaunti ya Mombasa imepuuzilia mbali uvumi kuhusu kupotea kwa sehemu za siri za wanaume, ikisema madai hayo si ya kweli.

Akizungumza kwa niaba ya idara hiyo, Kamishna wa Kaunti, Mohamed Nur, amesema uvumi huo ni njama inayotumiwa na magenge ya wahalifu kuwaibia wananchi.Ameongeza kuwa watu watatu wanazuiliwa kuhusiana na tuhuma hizo na kuonya kuwa yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wao, wanaharakati wa haki za binadamu wamekosoa hatua hiyo, wakisema imezua taharuki na kusababisha ukiukaji wa haki za binadamu, huku baadhi ya vijana wasio na hatia wakijeruhiwa na wengine kupoteza maisha.

Naye Francis Auma wa shirika la Muhuri amesema uvumi huo unasambazwa na baadhi ya waganga wa kienyeji kwa lengo la kujitangaza na kujinufaisha kifedha.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *