By Hassan Pojo

Shamra shamra na mbwembwe za kuanzia kwa mashindano ya Kitaifa ya Tong-Il Moo-Do kwa vijana yanayotarajiwa kuanza siku tano zijazo zimeanza, huku wanamichezo chipukizi kutoka sehemu mbalimbali za Kenya wakijiandaa kushiriki katika kinyang’anyiro hicho kitakachofanyika tarehe 18 na 19 Julai mwaka 2026.
Mtanange wa Kamoti Junior Super Cup makala ya tatu yanaendelea kutoa burudani katika eneobunge la Rabai Kaunti ya Kilifi huku timu mbalimbali zikijiandaa kuwania nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali.
Katika ratiba iliyotolewa na waandalizi, kutakuwa na mchezo mmoja wa hatua ya 16 bora utakaochezwa Jumamosi tarehe 18 Julai 2026, ambapo Hotspurs FC itavaana na United Kings kuanzia saa tisa alasiri katika Uwanja wa Lugwe.
