Idara ya mahakama imesisitiza kuwa sheria inawapa majaji mamlaka ya kutoa uamuzi mbadala tofauti na adhabu zilizopendekezwa kisheria, huku hakimu mkuu wa mahakama ya Mariakani Kimani Mburu akieleza kuwa kutoeleweka huku kumesababisha wananchi kushangaa hukumu nyepesi au dhamana kwa baadhi ya washukiwa, na akawahimiza wakaazi kutembelea mahakama kupata ufafanuzi wa kisheria.
wakati huo huo wakaazi wakiongozwa na Jackline Mueni walilalamikia ongezeko la dhulma dhidi ya watoto na kutaka sheria ichukue mkondo wake, huku Mburu akisisitiza ushirikiano wa washikadau kushughulikia kesi hizo kwa haraka na Fatuma Dzame akitoa wito wa mipango ya pamoja na ushauri ili kutafuta suluhu mbadala za migogoro ya kijamii.
