Maelfu Wanufaika na Huduma Mashinani Uwanja wa Tononoka Mombasa

Share this to

Maelfu ya wakaazi wa Mombasa wamejitokeza katika uwanja wa Tononoka kunufaika na huduma mashinani zilizoandaliwa na Wakfu wa Lulu la Jamii kwa ushirikiano na Huduma Center, wakieleza kuridhishwa na hatua hiyo kwani imepunguza muda na gharama za kupata huduma kama vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho, good conduct na huduma za afya.

Mwanzilishi wa wakfu huo, Lulu Hassan, amesema mwitikio mkubwa unaonyesha haja ya kuanzishwa kwa vituo zaidi vya Huduma Center kaunti ya Mombasa, kauli iliyoungwa mkono na msimamizi wa Huduma Center Mombasa, Harrison Yogo, huku wananchi wakihimizwa kujitokeza kwa wingi kunufaika na huduma hizo za bure.


Share this to

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *