madereva waandamana jomvu,kuulaani msongamano wa matrela

Share this to

Wakaazi wa Jomvu na wafanya biashara wanalalamikia msongamano wa malori Unao shuhudiwa kwenye barabara ya Madafuni na Jomvu mikanjuni.


Wakizungumza na wanahabari wamedai kwamba barabara hiyo huwa na msongamano mkubwa ambao hutatiza watoto wa shule na wale wanao kimbuzwa kwenye hospitali ilioko katika eneo hilo.


Wameomba uongozi uliopo katika eneo hilo kujitahidi na kuona kwamba tatizo hilo Lina shugulikiwa kikamilifu kuona kuwa linamalizwa.
Aidha vijana kutoka eneo hilo wameomba wenye makampuni katika kuwapa ajira ya kusaidia kuweka mpangilio muafaka wa malori hayo kuona kuwa hautakuwa na foleni kwenye barabara hiyo.


Kwa upande wao vijana walioko katika sekta ya uchukuzi wa matatu wamedai kwamba shuguli zao zimekuwa ngumu kutokana na msongamano unaoshuhudiwa.


Wakati huo huo waendesha boda boda wamedai kwamba foleni hiyo husababisha vijana wengi kuhusika na ajali za mara kwa mara.


Share this to

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *