Kadzo Catherine Ni Mwenye Tabasamu Baada Ya Mbunge Wa Jomvu Badi Twalib Kuingilia Kati Na Kufufua Ndoto Yake Ya Kujiunga Na Shule Ya Upili Ya Mama Ngina.
Hii Ni Baada Ya Juhudi Za Mzazi Wake Kigonga Mwamba Jambo Lililopelekea Walimu Wa Shule Hiyo Akiwemo David Mtugi Kusaka Usaidizi Mbalimbali.
Afisi Ya Mbunge Wa Jomvu Badi Twalib Ikiongozwa Na Mwenyekiti Wa Kamati Ya Cdf Owen Ogonda Imeahidi Kumuunga Msichana Huyo Katika Ufadhili Wa Masomo Ulioanzizshwa Na Mbunge Huyo Miaka Michache Iliyopita.
Aidha Mmoja Wa Maafisa Katika Ofisi Hiyo Asma Mohammed Amemuasa Catherine Kuzingatia Masomo Yake Na Kutojiingiza Katika Masuala Yasiyo Na Tija.
Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Badi Twalib Edith Mwova Pamoja Na Mzazi Wa Catherine Wamemshukuru Kiongozi Huyo Kwa Kuingilia Kati Na Kuwashika Mkono.
