Share this to

Spika wa Seneti, Amason Kingi, amesema ukosefu wa umoja miongoni mwa viongozi wa Pwani, hasa wakati wa uchaguzi, umechangia kuchelewesha maendeleo ya ukanda huo na kudhoofisha ushawishi wake katika siasa za kitaifa.

Akizungumza katika hafla ya kisiasa Pwani, Kingi alisema viongozi wa eneo hilo wanapaswa kuweka kando tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha maendeleo na kuongeza sauti ya ukanda huo katika masuala ya kitaifa.

Alisema tayari viongozi wa Pwani wameanza juhudi za kuwaunganisha viongozi wote wa ukanda huo ili kuzungumza kwa sauti moja, akisema hatua hiyo itasaidia Pwani kupata nafasi kubwa zaidi katika maendeleo na maamuzi ya kitaifa.

Wakati huo huo, Kingi alipuuza madai yanayosambazwa mitandaoni kwamba serikali ya Rais William Ruto haijatekeleza miradi ya maendeleo katika Pwani. Alisema serikali ya sasa imeanzisha na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika ukanda huo, akiwataka wananchi kutegemea taarifa rasmi badala ya uvumi.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Seneta wa Mombasa, Mohammed Faki, ambaye aliwataka wakazi wa Pwani kuendelea kumuunga mkono Rais William Ruto, akisema utekelezaji wa miradi ya maendeleo unapaswa kuwa msingi wa maamuzi yao ya kisiasa.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *