Share this to

By:Hassan Pojjo

Mgombea wa Ubunge wa Jomvu, Karisa Nzai Munyika, amekutana na wakazi wa eneo la Maganda walioathiriwa na mradi wa Reli ya Kisasa (MGR), ambapo alisikiliza malalamiko yao kuhusu kucheleweshwa kwa fidia na kuahidi kufuatilia kwa karibu suala hilo.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Munyika alisema amepokea maoni na changamoto za wakazi hao na kuahidi kushirikiana na mamlaka husika ili kuhakikisha walioathiriwa wanalipwa fidia yao kwa haki na kwa wakati.

Alisisitiza kuwa wananchi waliopoteza makazi au mali zao kutokana na mradi huo wanapaswa kushughulikiwa kwa heshima na bila kucheleweshwa na taratibu za kiutawala.

Mbali na suala la fidia, Munyika alisema amefurahishwa na mapokezi aliyopata kutoka kwa wakazi wa Maganda, akibainisha kuwa mazungumzo yao yalihusu pia maendeleo ya Jomvu, mshikamano wa jamii na umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi na wananchi katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wao, baadhi ya wakazi waliomba mchakato wa fidia uharakishwe, wakisema suala hilo limekuwa likisubiriwa kwa muda mrefu na limeathiri maisha ya familia nyingi.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *