Utafiti Wafichua Wasiwasi wa Wananchi Kuhusu Mwelekeo nchini Kenya  Huku Chama cha Linda Mwananchi na Sifuna akipata Umaarufu Mkubwa
Share this to

NAIROBI, Kenya

Msimamizi wa Shirika la Swiss Poll International akipeana taarifa ya ripoti.Picha naTeryani Mwadzaya

Utafiti mpya wa kitaifa uliotolewa na shirika la Swiss Poll Int. unaonyesha taswira ya hisia za wananchi wanaohisi nchi haiendi katika mwelekeo unaofaa, jambo linalodhihirika kupitia mabadiliko makubwa ya kisiasa na ukuaji wa kasi wa chama cha Linda Mwananchi cha Edwin Sifuna.

Hali hii ya kutoridhishwa na mwenendo wa mambo nchini imewasukuma wapiga kura wengi, hasa katika maeneo ya mijini na Magharibi mwa Kenya, kutafuta mbadala wa kisiasa na kiuchumi ambapo katika matokeo ya kura za maoni, chama cha Linda Mwananchi na mpeperusha bendera wake  Edwin Sifuna amepata uungwaji mkono mkubwa katika maeneo yenye changamoto kubwa za kiuchumi na ajira

Edwin Sifuna akiwa na wananchi katika rally za chama cha Linda Mwananchi.File Photo.

Ripoti hio inaonesha Edwin Sifuna anaongoza kwa kura za urais katika eneo la Magharibi akipata asili mia 35.8% na katika  jiji la Nairobi akipata asili mia 32.3%. Kasi hii inatafsiriwa kama ujumbe mzito kutoka kwa wananchi wanaotaka mabadiliko ya uongozi na utawala huku chama cha  Linda Mwananchi kikipata asili mia 33.4% katika maeneo ya Magharibi na asilimia 20.4% katika jiji la Nairobi, ikionyesha jinsi wananchi wanavyokiweka chama hicho kama sauti kuu ya upinzani na mbadala wa uongozi uliopo.

Ingawa wimbi la wananchi wanaotaka mabadiliko linakua mijini, maeneo mengine ya nchi yanaendelea kushikilia mwelekeo wa sasa au kuunga mkono viongozi wa kikanda ambapo chama cha UDA kikiongozwa na Rais William Ruto kinaendelea kuongoza katika Bonde la Ufa kwa asili mia huku Rais Rito akipata asili mia 64.6% katika maoni ya urais urais na chama cha UDA kikipata asli mia 56.8%

Baadhi ya waundaji maudhui wakiwa na wenyeji wao wa shirika la UNESCO katika chuo cha Agakhan jijini Nairobi kufunzwa kupeana habari au ujumbe katika maitandaom ya kijamii kwa kuzingatia sheria za usawa na kutosambaza habari potovu mitandaoni.Picha na Teryani Mwadzaya

Hali kadhalika wananchi wamesema kuwa kuongezeka kwa juhudi za kujitafutia riziki nje ya ajira za serikali au sekta rasmi imeongezeka na kuokana na Data za Swiss Poll Int. na BAKE ,Bloggers Association of Kenya zinaonyesha jinsi vijana na waundaji maudhui (content creators) wanavyopambana kujikimu.

Haya yanajiri huku shirika la Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni ,UNESCO likishirikisha waundaji maudhui kutoka nchi 15 barani Africa kuwafunza jinsi ya kuandaa habari kwa uangalifu  na kutathmini chanzo chake kabla ya kusambaza mitandaoni huku kauli mbiu ya warsha hio ikiwa sisi oste tuna nafasi ya kutekeleza katika jamii kuhakikisha habari za kweli zimesambazwa.


Share this to

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *