By:Athuman Luchi voiced by Farida Ali

Bweni la wanafunzi katika Markaz Al Abraar Islamic Centre, iliyoko eneo la Milalani, Msambweni, Kaunti ya Kwale, limeteketea kwa moto na kuungua kabisa.
Kwa mujibu wa taarifa, moto huo uliteketeza bweni lote pamoja na mali zote zilizokuwa ndani, zikiwemo Masaaf,mashuka, magodoro, nguo, vitabu na chakula cha wanafunzi. Hakuna chochote kilichofanikiwa kuokolewa.
Hakuna taarifa za majeruhi zilizoripotiwa kufikia sasa, huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijabainika.
Mamlaka husika zinatarajiwa kuanza uchunguzi kubaini chanzo cha mkasa huo, wakati viongozi, wadau na wasamaria wema wakihimizwa kujitokeza kutoa msaada kwa wanafunzi walioathirika ili waweze kurejea katika masomo yao kwa haraka.
