By:Hassan Pojjo

Mashindano ya Kamoti Junior Super Cup makala ya tatu yanaingia hatua ya robo fainali, huku timu nane bora zikitarajiwa kushuka dimbani Jumapili, Julai 26, kuwania tiketi ya kutinga nusu fainali.
Katika mechi hizo, Red Scorpion FC itachuana na Young Strikers FC katika Uwanja wa Mgala, huku Lexcon FC ikivaana na M’Barakani FC katika Uwanja wa Lugwe. Mechi zote zitaanza saa 9:00 alasiri, huku waandaaji wakiwahimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi na kudumisha amani pamoja na ushindani wa haki.
Na katika taarifa nyingine za michezo, mchezaji wa Busho FC, John Chigumba, maarufu kama John Jota, amejeruhiwa vibaya mkono wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Red Stars uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Jota alikimbizwa Hospitali ya Samburu kwa matibabu, huku uongozi wa Busho FC ukiomba wadau wa soka, mashabiki na wasamaria wema kujitokeza kuchangia gharama za matibabu yake. Timu hiyo imesema afya ya mchezaji huyo ndiyo kipaumbele kwa sasa, huku mashabiki wakimtakia apone haraka na arejee uwanjani.
