Share this to

By:Hassan Pojjo

Hispania imetwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Argentina bao 1-0 katika fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia leo.

Bao la ushindi lilifungwa na Ferran Torres katika muda wa nyongeza baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za kawaida.

Ushindi huo umeipa Hispania taji lake la pili la Kombe la Dunia, huku ukiihitimisha safari ya Argentina iliyokuwa ikitetea ubingwa.

Katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu, England iliichapa Ufaransa mabao 6-4 katika pambano la kusisimua na kujinyakulia medali ya shaba.

Michuano ya Kombe la Dunia 2026 imefikia tamati baada ya wiki kadhaa za ushindani mkali, huku Hispania ikidhihirisha ubora wake kwa kutwaa ubingwa na kuandika ukurasa mpya katika historia ya soka duniani.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *