Share this to

By:Hassan Pojjo

Shule ya Shikaadabu ya Likoni imefuzu kwa kishindo katika fainali za mashindano ya soka ya wasichana ya KPJSSA Mombasa County 2026 baada ya kuichapa Mlaleo ya Nyali mabao 6-0 kwenye nusu fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya St. Charles Lwanga.

Shikaadabu ilitawala mchezo kuanzia dakika za mwanzo, ikionyesha kiwango cha juu cha ushambuliaji na kuandika ushindi mkubwa unaoiweka hatua moja tu kutoka kutwaa ubingwa wa kaunti.

Na katika Ligi ya MSA Premier, Shimo Annex FC imeendeleza ubabe wake baada ya kuichapa Magongo Rangers mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Refinery, Changamwe.

Kipa Geofrey Lowo aliifungia Shimo Annex bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti, kabla ya Steven Chareli kufunga bao la pili dakika ya 82 na kuhitimisha ushindi huo muhimu.

Matokeo hayo yanaifanya Shimo Annex kuendelea kuimarisha nafasi yake kwenye mbio za ubingwa wa Ligi ya MSA Premier, huku Magongo Rangers wakilazimika kujipanga upya kuelekea mechi zijazo.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *