Share this to

By:Hassan Pojjo

MASHABIKI wa Arsenal katika eneo la Chaani, Changamwe kaunti ya Mombasa, wamefanya shangwe na nderemo baada ya timu yao kuanza msimu wa 2026/27 kwa kishindo, ikiichapa Manchester City mabao 3-0 na kutwaa Community Shield.

Voiced Package

Mashabiki hao wakiongozwa na Liban Abdkadir, walizunguka mitaa ya Chaani wakisherehekea ushindi huo, huku wakionyesha imani kubwa na kikosi cha kocha Mikel Arteta kuelekea msimu mpya.

Sherehe hizo zimekuwa sehemu ya utamaduni wa mashabiki hao, ambao hujumuika mitaani kila Arsenal inapopata ushindi mkubwa.

Arsenal ilifungua ukurasa wa mabao mapema sana katika mchezo huo uliochezwa Jumapili katika uwanja wa Principality Stadium mjini Cardiff, ambapo Riccardo Calafiori alifunga ndani ya sekunde 24 pekee.

Kai Havertz aliongeza bao la pili dakika ya 28, kabla ya nahodha Martin Ødegaard kufunga la tatu mapema kipindi cha pili na kuipa Arsenal ushindi wa mabao 3-0.

Winga mpya Christos Tzolis pia alikuwa na mchango mkubwa, akitoa pasi mbili za mabao katika ushindi huo.

Kwa Manchester City, huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa mashindano chini ya kocha mpya Enzo Maresca, baada ya kuchukua mikoba kufuatia kuondoka kwa Pep Guardiola.

Ushindi huo umeipa Arsenal mwanzo mzuri wa msimu na kuongeza matumaini miongoni mwa mashabiki wake kwamba kikosi hicho kinaweza kuwania mataji zaidi msimu huu.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *