Share this to

By:Alii Vincent

Siasa za ukabila zimeendelea kuzua mjadala katika Kaunti ya Kilifi huku joto la kisiasa likiongezeka kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, viongozi kutoka Eneo Bunge la Rabai wakionya dhidi ya kauli zinazoweza kugawa wananchi.

Aliyekuwa Diwani wa Wodi ya Kaliang’ombe, Said Charo, amekosoa matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara, Aisha Jumwa, akidai kuwa yanaweza kuchochea migawanyiko kwa kuashiria kuwa jamii fulani ni bora kuliko nyingine.

Charo amesema Mkoa wa Pwani unapaswa kuendelea kudumisha mshikamano na kukataa siasa za chuki na utengano, hasa wakati huu ambapo shughuli za kisiasa zinaendelea kushika kasi kuelekea uchaguzi mkuu.

Aidha, amefananisha matamshi hayo na kauli zilizowahi kutolewa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, akisema siasa zinazojengwa kwa misingi ya ukabila zinaweza kuwafanya wananchi kuchagua viongozi kwa kabila badala ya uwezo, uadilifu na utendaji wao.

Kauli za Charo zinajiri siku chache baada ya baadhi ya viongozi wa Pwani kuelezea wasiwasi wao kuhusu matamshi ya kisiasa yanayodaiwa kuhatarisha umoja wa kitaifa na mshikamano wa wananchi.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *