Share this to

By:Alii Vincent

Huku joto la Uchaguzi Mkuu wa 2027 likizidi kupanda, viongozi wa dini chini ya mwavuli wa Baraza la Makanisa Nchini (NCCK) wameonya dhidi ya matumizi ya fedha na dini kama nyenzo za kushawishi wapiga kura, wakisema hali hiyo inahatarisha demokrasia nchini.

Akiwasilisha ripoti ya kitaifa kuhusu athari za fedha na dini katika maamuzi ya wapiga kura, Mwenyekiti wa NCCK Kanda ya Pwani, Askofu Dkt. Peter Mwero, alisema umaskini na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana umewafanya kuwa rahisi kushawishiwa na wanasiasa, huku wengine wakitumiwa kuchochea vurugu za kisiasa.

Askofu Mwero pia amekosoa tabia ya baadhi ya wanasiasa kutumia madhabahu ya makanisa kama majukwaa ya kampeni, akisisitiza kuwa maeneo ya ibada yanapaswa kubaki sehemu za kuhubiri amani, maadili na mshikamano.

Viongozi hao wamewahimiza wananchi, hususan wanawake na vijana, kutokubali kuuza kura zao kwa manufaa ya muda mfupi, wakisisitiza kuwa maamuzi wanayofanya wakati wa kupiga kura yana athari za muda mrefu kwa maendeleo ya taifa.

Aidha, wamezitaka taasisi za kidini kuimarisha elimu ya uraia ili kuwajengea wananchi uwezo wa kufanya maamuzi huru na kuchagua viongozi wenye uadilifu, maadili na uwajibikaji.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *