By:Hassan Pojjo

Tatizo la maji limeendelea kuwa changamoto kubwa kwa wakazi wa Jomvu, huku mwanasiasa anayewania ubunge wa eneo hilo, Karisa Nzai Munyika, akisema juhudi za kupata suluhisho la kudumu zinaendelea kupitia mazungumzo na taasisi mbalimbali zinazohusika.
Karisa amesema mazungumzo hayo yanatoa matumaini ya kupatikana kwa suluhisho la kudumu ili kuhakikisha wakazi wanapata huduma ya maji safi kwa uhakika.

Wakati juhudi hizo zikiendelea, Karisa pamoja na timu yake walisambaza maji safi kwa wakazi wa Staff Area, Mikindani, eneo ambalo limekuwa likikabiliwa na uhaba wa maji.
Mbali na suala la maji, amesema anaendelea kushinikiza ukarabati wa barabara za mitaani zilizoharibika katika maeneo mbalimbali ya Jomvu, akisema hali hiyo imekuwa ikitatiza usafiri na shughuli za kiuchumi, hasa wakati wa mvua.

Amewataka wakazi wa Jomvu kuendelea kuunga mkono ajenda ya maendeleo na kushirikiana katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili.

Akihitimisha, Karisa amesisitiza kuwa maendeleo yanahitaji vitendo kuliko ahadi, akirejelea kauli mbiu yake ya “Kazi ni Kazi.”
