Share this to

By:Alii Vincent

Zaidi ya vitambulisho 1,500 bado havijachukuliwa katika eneo la Jomvu, Kaunti ya Mombasa, huku wakazi wakihimizwa kujitokeza kuvichukua pamoja na kadi zao za wapiga kura ili kujitayarisha mapema kwa Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza katika mkutano wa ushirikishwaji wa umma kuhusu upangaji wa miradi ya NG-CDF kwa miaka ya fedha 2026–2028 uliofanyika Jomvu, Mbunge wa Jomvu Badi Twalib alisema vitambulisho hivyo vitapelekwa katika maeneo ya mashinani ili kurahisisha wananchi kuvipokea.

Mbunge huyo pia aliwahimiza wananchi waliopoteza vitambulisho vyao kujitokeza kuomba vipya na kuhakikisha wanapata kadi zao za wapiga kura kwa wakati.

Badi alisema eneo la Pwani linatarajiwa kuandikisha wapigakura takriban milioni 3.5 kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, huku Jomvu ikilenga kuandikisha zaidi ya wapigakura 44,000.

Aidha, aliwataka wananchi kutokubali kushawishiwa kwa hongo au zawadi ndogo ili kuhamisha maeneo yao ya kupigia kura, akisisitiza kuwa kura ni haki ya msingi ya kila Mkenya na inapaswa kutumika kwa busara katika kuchagua viongozi.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *