Wakaazi wa eneo la Jomvu, Kaunti ya Mombasa, wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kama wapiga kura kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2027.
Akizungumza baada ya kukutana na jamii ya Wasomali mapema leo, Mbunge wa Jomvu, Badi Twalib, amesema yuko tayari kuwasilisha ombi kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ili kufanikisha zoezi la uandikishaji wa wapiga kura mashinani.
Wakati huo huo, Mbunge huyo amewahimiza vijana kuchukua hatua na kujiandikisha kwenye mradi wa serikali wa NYOTA, ili waweze kunufaika na fedha za kukuza biashara zinazotolewa na serikali.
Badi amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kutumia fedha hizo kuanzisha biashara halali, kujitegemea na kuboresha maisha yao.
Aidha, mbunge huyo amesema kuwa licha ya changamoto zinazokumba Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), ofisi yake iko mbioni kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanasajiliwa chini ya mpango huo. Ameeleza kuwa eneo bunge la Jomvu lina takribani shilingi milioni tisa zilizotengwa kwa ajili ya kugharamia hudu
