Ujenzi wa Daraja la Mwache Kwale Wafikia Asilimia 83

Share this to

Ujenzi wa Daraja la Mwache katika kaunti ya Kwale umefikia asilimia 83 ya ukamilishaji, huku serikali ikieleza kuwa mradi huo utaimarisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Kwale na Mombasa.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo, Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji, Bw. Julius Korir, amesema daraja hilo litachangia kwa kiasi kikubwa usambazaji wa maji ya kutosha katika maeneo hayo mawili.

Wakati huo huo, zaidi ya watu 3,000 wamehamishwa kutoka eneo la mradi huo, huku wizara ikisema kuwa imehakikisha mahitaji yao yote muhimu yanazingatiwa.

Aidha, ujenzi wa miundombinu muhimu ikiwemo shule, hospitali na kituo cha polisi kwa ajili ya wananchi waliohamishwa uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji.


Share this to

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *