Share this to

By:Hassan Pojjo

Shirika la Pwani Youth limeungana na washirika wa maendeleo, wafadhili na wadau mbalimbali kutoka barani Afrika katika mkutano unaofanyika wiki hii kuadhimisha miaka 20 ya ushirikiano na mafanikio, huku ukilenga kuweka mikakati ya maendeleo kwa kipindi cha miaka 20 ijayo.

Voiced Package

Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa mashirika ya vijana, watunga sera na washirika wa maendeleo kujadili mbinu mpya za kuwawezesha vijana, kukuza ubunifu na kuimarisha miradi yenye manufaa kwa jamii za Afrika.

Kupitia ushiriki wake, Pwani Youth imesema inalenga kuhakikisha sauti za vijana kutoka ukanda wa Pwani na Kenya kwa ujumla zinawakilishwa katika mijadala ya kimataifa kuhusu maendeleo, ajira, uongozi na ubunifu.

Shirika hilo linaamini kuwa ushirikiano na wadau mbalimbali utafungua fursa zaidi za kiuchumi na kijamii kwa vijana, huku ukiimarisha nafasi yao katika maendeleo ya bara la Afrika.

Aidha, washiriki wanatarajiwa kubadilishana uzoefu, kuwasilisha miradi bunifu na kujenga ushirikiano utakaowezesha utekelezaji wa programu za kuwawezesha vijana katika miaka ijayo.

Mkutano huo unaongozwa na kaulimbiu #Segal2026, #TheNextBeat, #Youthnaplanke na #Changemaker4Life, zinazosisitiza nafasi ya vijana kama chachu ya mabadiliko na maendeleo endelevu barani Afrika.

Pwani Youth imesisitiza kuwa ushiriki wake katika mkutano huo ni hatua muhimu ya kupanua mtandao wa ushirikiano na kuimarisha ajenda ya uwezeshaji wa vijana kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *