Share this to

By:Robert Mutasi

Mwinjilisti Richard Nyamunyamu kutoka Kaunti ya Nyamira amepokea kiti cha magurudumu kinachoendeshwa kwa umeme baada ya video yake akiimba pamoja na binti yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kiti hicho kilitolewa na wahisani kutoka Kaunti ya Uasin Gishu katika hafla iliyofanyika Eldoret, wakisema kitamwezesha kusafiri kwa urahisi zaidi anapoendelea kuhubiri injili na kuimba.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Nyamunyamu aliwashukuru wahisani akisema kiti hicho kimebadilisha maisha yake na kitamrahisishia kutekeleza huduma yake kwa ufanisi zaidi.

Wahisani hao wamewataka Wakenya kuendelea kuwasaidia watu wenye ulemavu, wakisema mshikamano wa jamii unaweza kubadilisha maisha ya wengi.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *