By:Hassan Pojjo

Kiungo wa timu ya taifa ya wasichana chini ya miaka 17, Junior Starlets, Mwanakombo Bakari, anaendelea kung’ara na kujizolea sifa kutokana na kiwango chake bora cha uchezaji.
Mwanakombo ameendelea kuwa nguzo muhimu katika safu ya kiungo kwa uwezo wake wa kumiliki mpira, kutoa pasi za uhakika na kuvunja mashambulizi ya wapinzani. Utulivu wake, nidhamu na uwezo wa kusoma mchezo vimemfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa zaidi na benchi la ufundi.
Mashabiki na wadau wa soka wameendelea kuvutiwa na uwezo wake wa kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji, huku wengi wakiamini kuwa akidumisha kiwango hicho ana nafasi kubwa ya kuitumikia timu ya taifa ya wanawake, Harambee Starlets, katika siku zijazo.
Kwa sasa, Mwanakombo anaendelea kuthibitisha kuwa ni mmoja wa viungo wenye mustakabali mkubwa katika soka la wanawake nchini.
Mashindano ya Kamoti Junior Super Cup makala ya tatu sasa yanaingia hatua ya robo fainali, huku timu nane bora zikitarajiwa kushuka dimbani Jumapili, Julai 26, 2026, kuwania tiketi ya kutinga nusu fainali.
Kwa mujibu wa ratiba ya waandaaji, mechi mbili zitachezwa kuanzia saa 9:00 alasiri katika viwanja viwili tofauti vya Kaunti ya Kilifi.
Katika Uwanja wa Mgala, Red Scorpion FC itavaana na Young Strikers FC katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Wakati huohuo, Lexcon FC itamenyana na M’Barakani FC katika Uwanja wa Lugwe, huku kila timu ikisaka ushindi na nafasi ya kuendelea na mbio za ubingwa.
Waandaaji wanasema mashindano hayo yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuibua na kukuza vipaji vya soka kwa vijana katika ukanda wa Pwani, huku yakivutia mashabiki, makocha na maskauti wanaofuatilia vipaji vinavyochipukia.
Mashabiki wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hizo muhimu, huku wakihimizwa kudumisha amani, nidhamu na ushindani wa haki viwanjani.
Kwa ufupi ratiba ya robo fainali ni kama ifuatavyo:
- Red Scorpion FC dhidi ya Young Strikers FC – Saa 9:00 alasiri, Uwanja wa Mgala.
- Lexcon FC dhidi ya M’Barakani FC – Saa 9:00 alasiri, Uwanja wa Lugwe.
