Share this to

By:Robert Mutasi & Farida Ali

Serikali imetakiwa kuajiri masheikh na maimam katika hospitali zote za umma ili kuwaombea wagonjwa na kuwapa huduma za kidini.

Wito huo umetolewa na Sheikh Abu Qatada alipohudhuria mkutano wa masheikh uliofanyika Ikulu ya Nairobi.

Aidha, ameiomba serikali kusitisha masomo ya ziada wakati wa likizo za shule ili kuwapa watoto nafasi ya kuhudhuria madrasa na kuimarisha elimu ya dini.

Vilevile, masheikh hao wamemtaka Rais kufanya marekebisho katika mfumo wa Elimu ya Ujuzi (Competency-Based Education – CBE), wakidai kuwa mfumo huo umepuuza na kutenga masomo ya dini.

Sheikh Abu Qatada pia amemtaka Rais kusimamia gharama za maimam kutoka kila kaunti ili kutekeleza ibada za Umra na Hija, akisema wengi wao hushindwa kutokana na gharama kubwa za safari hizo.

Kwa upande mwingine, viongozi hao wa dini wamemtaka Rais kuhakikisha misikiti inapatiwa hati miliki ili kulinda umiliki wa maeneo ya ibada na kuondoa migogoro ya ardhi.

Masheikh hao pia walimpongeza Rais kwa juhudi zake za maendeleo na ushirikiano wake na viongozi wa dini.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *