Share this to

By:Alii Vincent

Malalamiko kuhusu huduma za matibabu kwa walimu kupitia Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) yameanza kupungua, baada ya walimu kuanza kupata huduma katika baadhi ya hospitali za umma nchini.

Akizungumza na wanahabari, Katibu wa Chama cha Walimu Nchini (KNUT) tawi la Mombasa, Ahmed Kombo Ahmed, alisema walimu wameanza kupokea huduma za afya kupitia mfumo wa SHA, hatua aliyosema imeleta afueni kwa walimu waliokuwa wameathirika na changamoto za awali.

Hata hivyo, Kombo ameisihi serikali kupitia upya masharti ya kiwango cha fedha kinachotengwa kwa matibabu ya kila siku, akisema hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa walimu na wafanyakazi wengine wa umma.

Wakati huohuo, ameitaka serikali kutekeleza nyongeza ya mishahara ya walimu kwa awamu moja badala ya mfumo wa sasa wa nyongeza za hatua kwa hatua.

Aidha, Kombo ametoa wito wa kuongezwa kwa ufadhili wa michezo katika shule za msingi kote nchini ili kutoa fursa sawa kwa wanafunzi kutambua na kukuza vipaji vyao mapema.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *