Share this to

By:Hassan Pojjo

Junda United imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coast United katika mechi ya Ligi ya FKF Mombasa County, na kujikusanyia alama tatu muhimu huku Coast United ikiondoka bila pointi.

Junda United ilitawala sehemu kubwa ya mchezo, ikitumia vyema nafasi ilizozipata kufunga mabao mawili yaliyowahakikishia ushindi muhimu. Kwa upande wake, Coast United ilijitahidi kusaka matokeo licha ya kutegemea kikosi chake cha vijana, lakini ilishindwa kupenya safu imara ya ulinzi ya wapinzani wao.

Baada ya mchezo, viongozi wa Coast United waliikubali matokeo hayo kwa moyo wa kiushindani na kuipongeza Junda United kwa ushindi huo, huku wakiwatakia mafanikio katika mechi zijazo.

Licha ya kipigo hicho, Coast United imesema imepata mafunzo muhimu yatakayosaidia kuboresha kiwango cha timu. Benchi la ufundi limeahidi kufanya tathmini ya makosa yaliyojitokeza na kuyafanyia kazi katika mazoezi kuelekea duru ya pili ya ligi.

Kocha pamoja na viongozi wa klabu wameeleza kuwa bado wana imani na kikosi chao cha vijana, wakisisitiza kuwa kwa nidhamu, kujituma na ushirikiano, timu hiyo itarejea ikiwa imara zaidi.

Vilevile, klabu hiyo imewashukuru mashabiki, viongozi na wadau wake kwa kuendelea kuipa sapoti licha ya matokeo hayo, ikisema mchango wao unaipa timu motisha ya kuendelea kupambana.

Sasa Coast United inaelekeza nguvu zake katika maandalizi ya duru ya pili ya Ligi ya FKF Mombasa County, ikiwa na matumaini ya kurejea kwa ushindani mkubwa na kuboresha nafasi yake kwenye msimamo wa ligi.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *