Share this to

By:Hassan Pojjo

Harambee Starlets imeanza kwa mguu mbaya kampeni yake ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (AWCON 2026) baada ya kuchapwa mabao 4-0 na wenyeji Morocco katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A uliochezwa jijini Rabat.

Morocco ilitawala mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho, huku kikosi cha kocha Beldine Odemba kikishindwa kupata majibu dhidi ya wenyeji hao. Kufuatia matokeo hayo, Kenya italazimika kusaka ushindi katika mechi zake zilizobaki dhidi ya Algeria na Senegal ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali.

Wakati huo huo, maandalizi ya Joha Foundation Tournament yanaendelea kushika kasi baada ya viongozi wa vilabu 25, vikiwemo Lexcon FC, Chui FC, Power FC, Bengo FC, Soccer Friends FC na Mazeras City FC, kukutana kujadili maandalizi ya mashindano hayo.

Katika mkutano huo, ilikubaliwa kuwa kila klabu itapatiwa mpira mmoja wa mashindano, huku mfadhili akiahidi jezi, medali, vikombe, vifaa vya michezo na fedha taslimu kwa washindi. Kiwango cha fedha za zawadi kinatarajiwa kutangazwa katika mkutano utakaofanyika Agosti 2, 2026, kabla ya kuanza rasmi kwa mashindano.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *