By:Hassan Pojjo

Timu ya Green Eagles imefuzu hatua ya robo fainali ya mashindano ya SISI NI DOLA CUP 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtwapa All Stars katika mchezo wa hatua ya mtoano.
Bao pekee la mchezo lilifungwa mapema na mshambuliaji Paul Otieno, aliyemalizia kwa ustadi pasi ya Ali Washe, na kuipa Green Eagles tiketi ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo.
Kutokana na mchango wake mkubwa, Paul Otieno alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi (Man of the Match) baada ya kufunga bao lililoamua matokeo.
Kwa ushindi huo, Green Eagles imejiunga na timu nyingine zilizofuzu hatua ya robo fainali, huku ikiongeza matumaini ya kutwaa ubingwa wa SISI NI DOLA CUP 2026.
Mashindano hayo yanaendelea kushuhudia ushindani mkali, huku wadau na mashabiki wa soka nchini wakisubiri kwa hamu mechi za robo fainali.
