Share this to

By:Glory Mwagambo

Washikadau wa usalama, viongozi wa dini na jamii mjini Malindi wameungana kutafuta suluhu ya kudumu kwa ongezeko la uhalifu katika mitaa ya Mere na Ganda, Kaunti ya Kilifi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama na Amani Malindi, Athuman Ali, amesema visa vya uhalifu vinavyohusishwa na makundi ya vijana vimeathiri usalama na kudorora kwa shughuli za kiuchumi. Amewataka wazazi kushirikiana na vyombo vya usalama badala ya kuwaficha watoto wanaotafutwa kwa tuhuma za uhalifu.

Naye Askofu David Mole amesema wazazi wana jukumu la kuimarisha malezi, akieleza kuwa matumizi ya dawa za kulevya na mienendo kama disco matanga yamechangia kuongezeka kwa uhalifu miongoni mwa vijana.

Washikadau hao wamewahimiza vijana kujiepusha na uhalifu na badala yake kushiriki katika shughuli halali za kujipatia kipato ili kurejesha amani na usalama katika maeneo hayo.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *