Mbunge wa Jomvu, Badi Twalib, amesisitiza kuwa chama cha ODM bado kiko imara, licha ya kuondokewa na kinara wake.
Akizungumza na wanahabari, Badi amesema viongozi wa chama hicho wako mbioni kuhakikisha kuwa mambo yanawekwa sawa ndani ya ODM ili kuendelea kukiimarisha.
