Share this to

By:Hassan Pojjo

Shule ya St. Charles Lwanga imeibuka mabingwa wa mashindano hayo baada ya kuonyesha kiwango cha juu cha ushindani, nidhamu na uchezaji bora.

Ushindi huo umechangiwa na juhudi za wanafunzi, walimu, benchi la ufundi pamoja na uungwaji mkono kutoka kwa wazazi na wadau wa elimu.

Timu hiyo ilionyesha mchezo wa kuvutia katika hatua mbalimbali za mashindano na hatimaye kutwaa ubingwa.

Uongozi wa shule umepongeza wanafunzi kwa kujituma, ukisema utaendelea kuwekeza katika kukuza vipaji vya michezo sambamba na taaluma.

Wadau mbalimbali wa elimu pia wameipongeza shule hiyo kwa mafanikio hayo na kuwataka wanafunzi kuendeleza bidii katika michezo na masomo.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *