Share this to

By:Farida Ali

Serikali inatarajiwa kuzindua rasmi Kituo cha Kitaifa cha Kuratibu Huduma za Ambulansi wiki ijayo, hatua inayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika utoaji wa huduma za dharura nchini.

Kituo hicho kitakuwa kitovu cha uratibu wa magari ya kubeba wagonjwa kote nchini, kikihakikisha wagonjwa na waathiriwa wa ajali au majanga wanapata msaada kwa wakati bila kujali eneo walipo.

Kwa mujibu wa serikali, mfumo huo mpya utaunganisha huduma za ambulansi kutoka kaunti mbalimbali na taasisi za afya kupitia kituo kimoja cha kitaifa, jambo litakalorahisisha mawasiliano, kuongeza kasi ya mwitikio na kupunguza muda wa kusubiri huduma za dharura.

Uzinduzi huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mfumo wa afya nchini na kuhakikisha huduma za uokoaji zinawafikia wananchi kwa haraka zaidi wakati wa majanga, ajali za barabarani na dharura nyingine za kiafya.

Wakati huohuo, serikali imetangaza nambari mpya ya dharura 922, ambayo itatumika kote nchini kuomba huduma za ambulansi.

Wananchi wanahimizwa kuhifadhi nambari hiyo kwenye simu zao na kuitumia kwa dharura halisi, huku serikali ikisisitiza kuwa kila sekunde ina umuhimu mkubwa katika kuokoa maisha.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *