Share this to

By:Athuman Luchi

Wakaazi wa Mombasa wametakiwa kuzaa watoto wengi ili kuongeza idadi ya wakazi na, hatimaye, kuongeza idadi ya wapiga kura katika siku zijazo.

Akizungumza, Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Nassir, alisema ongezeko la idadi ya watu linapaswa kwenda sambamba na uwekezaji katika huduma za afya na elimu ili kuhakikisha watoto wanapata fursa bora za maisha.

Alisema serikali ya kaunti tayari inatoa huduma za matibabu kwa watoto bila malipo, elimu ya chekechea bila ada na mpango wa chakula cha mchana katika shule zote za umma.

Aidha, amesema serikali yake inalenga kupanua uwekezaji katika sekta ya elimu, akieleza matumaini kwamba siku zijazo elimu itakuwa bila malipo ili kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kusoma.

Kauli hizo zinajiri wakati mataifa mbalimbali duniani yakiendelea kujadili sera za uzazi, ukuaji wa idadi ya watu na uwekezaji katika huduma za kijamii kama nguzo muhimu za maendeleo.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *