Share this to

Ngarambe za Mtwapa Premier League zinaendelea kushika kasi katika viwanja mbalimbali, huku timu zikionyesha ushindani mkali katika harakati za kusaka alama muhimu na kuboresha nafasi zao kwenye msimamo wa ligi.

Tukianzia katika uwanja wa Annex, Majaoni Young Star iliibuka na ushindi mwembamba wa bao moja bila majibu dhidi ya New Talent.

Bao pekee la mchezo lilitokana na kujifunga kwa beki wa New Talent, Hamza Suleiman, katika dakika ya 10, bao lililowapa Majaoni Young Star alama zote tatu.

Katika uwanja wa Mtwapa KP, Bomani FC iliibwaga Komboa FC kwa mabao mawili kwa moja.

Komboa FC walitangulia kupata bao kupitia kwa Jackbrek Ochieng, lakini Bomani FC waligeuza meza kupitia kwa mabao ya Gideon Ngundo na Kelvin Ngumbao.

Mchezo huo pia ulishuhudia mwamuzi akitoa kadi za njano kwa Kingi Kitsao wa Komboa FC na Gideon Ngundo wa Bomani FC kufuatia makosa ya uwanjani.

Katika pambano lililochezwa kati ya Kilifi TRS na Laliga FC, timu hizo zilitoka sare ya bao moja kwa moja.

Laliga FC walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu kupitia kwa Amani Chengo katika dakika ya 38, kabla ya Donald Anzani kuisawazishia Kilifi TRS katika dakika ya 58.

Mchezo huo pia ulikuwa na ushindani mkali, huku waamuzi wakitoa kadi nne za njano. Kwa upande wa Kilifi TRS, Joseph Anguyo na Morris Nenga waliadhibiwa, huku John Magwaya na Mango Yusufu wakipewa kadi kwa upande wa Laliga FC.

Na katika uwanja wa Kanamai, Mvita Oil FC ilitoa onyesho la kuvutia kwa kuichapa Sunset FC mabao manne kwa bila.

Kepha Larrick alifunga bao moja, Phidel Onyango akang’ara kwa mabao mawili, huku Rilex Patrick akihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne.

Licha ya ushindi huo mnono, Kepha Larrick pia alionyeshwa kadi ya njano katika mchezo huo.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *