WAZAZI WASIOPELEKA WATOTO SHULE RABAI CHAO KIMOTONI

Share this to

Wazazi watakaokiuka agizo la Rais la kuwapeleka watoto wao kujiunga na shule za sekondari za juu katika eneo la Rabai huenda wakashtakiwa kwa kosa la kutelekeza watoto.


Kwa mujibu wa Chifu wa Rabai, Anthony Jao, tayari amewaagiza manaibu chifu pamoja na wazee wa mtaa kuorodhesha wazazi ambao watoto wao hawajajiunga na kidato cha kwanza baada ya kukamilisha mitihani ya

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Isaac Nyondo, Josephine Njagi, amewahimiza wazazi kuendelea kushirikiana na walimu ili kuboresha matokeo ya wanafunzi kwa kutimiza wajibu wao ipasavyo.


Kulingana na Mwalimu Njagi, zaidi ya wanafunzi 50 kutoka shule hiyo wamefanikiwa kupata nafasi katika shule za kitaifa. Amewasihi wazazi kuhakikisha watoto wao wanajiunga na shule hizo wanapofaulu kuendelea na masomo ya sekondari ya juu.


Share this to

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *