Share this to

By:Glory Mwagambo

Watu wenye ulemavu nchini wameitaka serikali na viongozi wa kisiasa kuhakikisha wanashirikishwa kikamilifu katika masuala ya kitaifa na kisiasa bila ubaguzi, wakisema bado wanakumbana na changamoto za kutengwa licha ya kuwa na haki sawa kama Wakenya wengine.

Voiced Package

Wakizungumza mjini Malindi, Kaunti ya Kilifi, viongozi wa watu wenye ulemavu walisema ni muhimu serikali ihakikishe wanapata huduma za umma kwa usawa, ikiwemo vitambulisho vya taifa na nyaraka nyingine muhimu zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi na maendeleo ya nchi.

Rais wa chama cha watu wenye ulemavu mjini Malindi alisema wataendelea kutetea haki za kundi hilo na kupinga vitendo vyovyote vya ubaguzi au unyanyasaji dhidi yao. Pia alitoa wito kwa serikali na viongozi waliochaguliwa kuhakikisha watu wenye ulemavu hawanyimwi haki zao za msingi.

Naye Stella Kadzo alisema watu wenye ulemavu bado hukumbana na changamoto wanapotafuta vitambulisho vya taifa na huduma nyingine za serikali. Alisisitiza kuwa wao ni raia wenye haki sawa na hawapaswi kubaguliwa kwa misingi ya ulemavu wao.

Kwa upande wake, Mvera Kahatso alitaka serikali, viongozi na jamii kwa ujumla kuwapa watu wenye ulemavu fursa sawa za ajira, maendeleo na uwezeshaji wa kiuchumi. Alisema hatua hiyo itawawezesha kujitegemea na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *