By:Hassan Pojo

Ngarambe za Kombe la Dunia 2026 yanaendelea kunoga huku hatua ya nusu fainali ikifikia tamati usiku wa leo.
Usiku wa jana, timu ya Uhispania ilitinga fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ufaransa katika mchezo uliopigwa jijini Arlington, Texas.
Uhispania ilionyesha gemu safi katika mchezo huo kwa kutawala sehemu kubwa ya mechi na kutumia vyema nafasi walizozipata.
Ushindi huo umeihakikishia nafasi ya kucheza fainali ya Kombe la Dunia, huku Ufaransa ikielekezwa kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu.
Leo Julai 15, macho ya dunia yataelekezwa kwenye nusu fainali ya pili ambapo England itavaana na Argentina katika pambano litakalofanyika jijini Atlanta.
Mshindi wa mchezo huo atafuzu moja kwa moja kucheza fainali dhidi ya Uhispania, huku atakayepoteza akitarajiwa kukutana na Ufaransa katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa kutokana na ukwasi wa vikosi vya pande zote mbili.
England imeonyesha kiwango kizuri tangu kuanza kwa mashindano hayo, huku Argentina nayo ikiongozwa na kikosi chenye uzoefu na uwezo mkubwa wa kushambulia.
Mashabiki wa soka duniani wanatarajia kushuhudia pambano kali litakaloamua nani atakayekamilisha ratiba ya fainali ya Kombe la Dunia 2026.
