Share this to

By:Hassan Pojjo

Mashindano ya Sisi Ni Dola Cup yanaingia hatua ya mwisho Ijumaa wiki hii, huku Alshifaa Media FC ikitarajiwa kukutana na Green Eagles katika mchezo wa fainali utakaochezwa kwenye uwanja wa Mombasa Sports Club.

Fainali hiyo inatarajiwa kuwa kivutio kwa mashabiki wa soka, baada ya timu hizo kuonyesha ushindani mkubwa na kufanikiwa kufuzu hadi hatua ya mwisho ya michuano hiyo.

Alshifaa Media FC itaingia uwanjani ikilenga kutwaa ubingwa pamoja na zawadi ya Sh milioni moja, huku Green Eagles ikiwa na dhamira ya kuzuia mpango huo na kuondoka na taji.

NYUNDO FC, AZZAM UNITED KUPIGANIA NAFASI YA TATU

Kabla ya fainali, Nyundo FC itamenyana na Azzam United siku ya Alhamisi katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu.

Timu hizo zitalenga kumaliza mashindano kwa ushindi na kujinyakulia zawadi ya Sh250,000.

SH1 MILIONI KWA BINGWA

Bingwa wa Sisi Ni Dola Cup ataondoka na kitita cha Sh milioni moja, huku mshindi wa pili akipata Sh500,000 na mshindi wa tatu Sh250,000.

Kwa mashabiki wa soka, macho yote yataelekezwa Mombasa Sports Club Ijumaa, wakati Alshifaa Media FC na Green Eagles zitakapokutana kuwania taji la Sisi Ni Dola Cup.

Bingwa: Sh1,000,000 | Mshindi wa pili: Sh500,000 | Mshindi wa tatu: Sh250,000


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *