Share this to

Serikali imeongeza kwa siku 30 muda wa utekelezaji wa oparesheni za usalama katika baadhi ya maeneo ya Kaunti ya Marsabit, kufuatia hali inayoendelea ya ukosefu wa usalama.

Kupitia Gazeti Rasmi la Serikali, Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen amesema maeneo yaliyotangazwa kuwa hatari yataendelea kuwa chini ya operesheni maalum za kiusalama kwa mwezi mmoja zaidi.

Sambamba na hatua hiyo, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja ameagiza wakazi wa maeneo husika waliomiliki silaha kuzisalimisha mara moja katika vituo vya polisi au ofisi za Utawala wa Kitaifa kwa hifadhi salama.

Serikali imesema silaha hizo zitarejeshwa kwa wamiliki halali mara tu tamko la maeneo hayo kuwa hatari litakapofutwa, huku ikisisitiza kuwa hatua hizo zinalenga kuimarisha usalama na kurejesha utulivu katika eneo la Marsabit.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *