Share this to

By:Alii Vincent

Viongozi wa serikali katika Eneo Bunge la Rabai, Kaunti ya Kilifi, wameitaka serikali kuu kuharakisha mchakato wa kupandisha hadhi baadhi ya kata ndogo kuwa lokesheni kamili ili kuboresha upatikanaji wa huduma za serikali kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kikao cha ushirikishwaji wa umma katika eneo la Kaliang’ombe, Chifu Anthony Jao alisema serikali tayari imeidhinisha kupandishwa hadhi kwa kata ndogo tatu kati ya nne zilizopendekezwa na viongozi wa eneo hilo.

Jao alisema baadhi ya kata ndogo zina wakazi zaidi ya 27,000 huku nyingine zikiwa na takriban wakazi 4,000 pekee, hali inayosababisha mgawanyo usio sawa wa kiutawala na kuongeza mzigo kwa maafisa waliopo.

Alisema kukamilika kwa mchakato huo kutarahisisha kuongezwa kwa maafisa wa utawala, kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi na kuimarisha utoaji wa huduma za serikali katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *