Share this to

By:Hassan Pojo

Mji wa Mariakani, Kaunti ya Kilifi, unatarajiwa kupata mabadiliko makubwa ya kiuchumi baada ya kutengewa miradi miwili mikubwa ya maendeleo.

Miradi hiyo ni ujenzi wa Lorry Park kwenye ekari 10 na Nyumba za Gharama Nafuu kwenye ekari 50, hatua inayolenga kuboresha usafiri, makazi na kukuza uchumi wa eneo hilo.

Lorry Park inatarajiwa kupunguza msongamano wa malori katika Barabara ya Mombasa–Nairobi na kuimarisha shughuli za usafirishaji, huku mradi wa nyumba ukilenga kuongeza upatikanaji wa makazi bora kwa wananchi.

Serikali na viongozi wa Kaunti ya Kilifi wanasema miradi hiyo itafungua nafasi za ajira, kuvutia uwekezaji na kuifanya Mariakani kuwa kituo muhimu cha biashara na usafirishaji katika ukanda wa Pwani.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *