Share this to

By:Hassan Pojjo

Mbunge wa Mvita, Mohammed Masoud Machele, ametembelea Gereza la Mombasa Remand, maarufu kama Jela Baridi, ambapo ameshuhudia Kamati ya Mvita NG-CDF ikikabidhi rasmi eneo la mradi wa ujenzi wa barabara za mawe (cabro) ndani ya gereza hilo.

Mradi huo unalenga kuboresha miundombinu ya ndani ya gereza kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma, kuimarisha usafiri wa ndani na kuboresha mazingira kwa wafungwa, maafisa wa magereza na wageni wanaotembelea kituo hicho.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Machele alisema Mvita NG-CDF itaendelea kushirikiana na taasisi za umma kutekeleza miradi ya maendeleo inayoboresha utoaji wa huduma na kuimarisha mazingira ya kazi kwa manufaa ya wananchi.

Kwa upande wake, uongozi wa Gereza la Mombasa Remand uliishukuru Mvita NG-CDF kwa kufadhili mradi huo, ukisema utasaidia kuboresha miundombinu ya gereza na kuongeza ufanisi wa shughuli za kila siku.

Ujenzi wa barabara za cabro unatarajiwa kuanza mara moja baada ya kukabidhiwa rasmi kwa eneo la mradi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuimarisha miundombinu ya taasisi za umma katika eneo bunge la Mvita.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *