Share this to

Wakazi wa Kisumu Ndogo mjini Malindi, Kaunti ya Kilifi, wameibua malalamiko kuhusu ujenzi wa kituo cha mafuta katikati ya makazi yao, wakihofia usalama wa maisha na mali zao.

Wakazi hao wameitaka NEMA pamoja na Serikali ya Kaunti kuingilia kati, wakidai kuwa mradi huo umeathiri biashara za kina mama waliokuwa wakitegemea eneo hilo kujipatia kipato.

Wanasema uwepo wa kituo hicho katika eneo lenye msongamano wa makazi unaweza kusababisha madhara makubwa endapo kutatokea ajali au moto.

Mmoja wa wakazi hao, Ann Wanjiru, amesema ujenzi huo umeongeza changamoto wakati wa msimu wa mvua, huku baadhi ya nyumba na biashara zikikumbwa na mafuriko.

Ameongeza kuwa licha ya kuwasilisha malalamiko katika ofisi ya manispaa, bado hajapata majibu.

Wakazi hao sasa wanaitaka Serikali ya Kaunti pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA) kuchukua hatua kuhusu suala hilo kabla madhara hayajatokea.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *