Share this to

Kilio cha uchafu wa majitaka kimeendelea kutawala maisha ya wakaazi wa Majengo jijini Mombasa, huku wakilalamikia hali ya mazingira inayoweka afya zao hatarini.

Mashimo ya majitaka yamekuwa yakifurika na kumwaga uchafu hadi ndani ya baadhi ya nyumba, hali inayowalazimu wakaazi kufunga milango na madirisha muda mwingi ili kujikinga na harufu kali na hofu ya magonjwa.

Wakaazi hao wanasema wamekuwa wakitoa malalamiko kwa muda mrefu bila kupata suluhisho, huku wakizitaka mamlaka husika, ikiwemo Serikali ya Kaunti ya Mombasa na taasisi za mazingira, kuchukua hatua za haraka.

Baadhi yao wanadai watoto wameathirika zaidi kutokana na kushindwa kucheza nje kwa uhuru kwa hofu ya kuambukizwa magonjwa.

Hadi sasa, juhudi za kupata kauli kutoka kwa maafisa wa afya na mazingira wa Kaunti ya Mombasa kuhusu hali hiyo bado hazijafanikiwa.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *