By:Hassan Pojjo

Timu ya Busho Ocean Stars imeendelea kuonyesha kiwango kizuri katika michuano ya Samba Sports Tournament, baada ya kupata matokeo mazuri katika michezo yake ya awali.
Busho Ocean Stars imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Aim Boyz, kabla ya kutoka sare ya 0-0 na Youngster FC. Katika mchezo mwingine, Busho Ocean Stars ilionyesha ubora mkubwa kwa kuifunga Vinyunduni Sports Society (VSS) mabao 3-0.
Matokeo hayo yanaifanya Busho Ocean Stars kuingia katika mchezo wake unaofuata ikiwa na matumaini ya kuendelea na mwenendo mzuri katika mashindano hayo.
LEO DIMBANI
Leo macho ya mashabiki wa soka yataelekezwa katika mchezo unaotarajiwa kuwakutanisha Busho Ocean Stars dhidi ya Birikani FC.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Busho Ocean Stars ikilenga kuendeleza kasi yake baada ya kupata ushindi katika michezo yake iliyopita.
Mashabiki wa soka wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya Samba Sports Tournament na kuzipa nguvu timu zao katika harakati za kutafuta ubingwa wa mashindano hayo.
