By:Hassan Pojjo

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rabai wanatarajiwa kupata nafuu ya upatikanaji wa maji baada ya Mbunge wa Rabai, Antony Kenga Mupe, kuzindua rasmi mradi wa kisima cha maji Jumamosi, Agosti 1, 2026.
Mradi huo unalenga kuhakikisha wanafunzi na walimu wanapata maji safi na salama, huku ukiboresha afya na mazingira ya kujifunzia.
Kenga amesema upatikanaji wa huduma muhimu kama maji ni msingi wa maendeleo, akiwataka wakazi kushirikiana katika kutekeleza miradi yenye manufaa kwa jamii.
Uzinduzi huo utafanyika katika Shule ya Sekondari ya Rabai, ambapo wananchi na wadau mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.
