
Walimu elfu ishirini wataajiriwa na Tume ya Kuajiri Walimu nchini, TSC, kwa ajili ya kufundisha katika Shule za Junior, kama sehemu ya kuimarisha utekelezaji wa mfumo wa elimu wa Umahiri, CBC.
TSC imesema maombi yatawasilishwa mtandaoni pekee kuanzia Agosti 18 hadi usiku wa manane wa Agosti 31, mwaka 2026,
Hatua hiyo inajiri wakati serikali ikijiandaa kuwaajiri walimu kwa masharti ya kudumu na ya pensheni, baada ya kutenga shilingi bilioni 13.1 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa zoezi hilo.
