
Gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja, ametangaza mpango wa kujenga reli ya kwanza ya chini kwa chini katika Jiji la Nairobi, mradi unaolenga kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri wa umma.
Akizungumza mbele ya Seneti, Sakaja alisema serikali ya kaunti imeidhinisha mfumo wa Nairobi Mass Rapid Transit System (NMRTS) wenye thamani ya dola bilioni 7.78.
Alisema reli hiyo itapita chini ya maeneo ya katikati ya jiji na kuunganishwa na njia za juu katika maeneo ya pembezoni, hatua itakayobadilisha mfumo wa usafiri jijini.
Sakaja alisema mipango ya reli hiyo imekuwa ikijadiliwa tangu mwaka 1948, 1972 na 2014, lakini haikufanikiwa kutekelezwa kutokana na changamoto za ufadhili na mipango.
Amesema lengo la mradi huo ni kuifanya Nairobi kuwa jiji la dakika 20, ambapo wakazi wataweza kufikia maeneo muhimu kwa muda mfupi zaidi.Sara Kimani Mwanga wa Kilele
