By:Hassan Pojjo

Nyota wa Arsenal Bukayo Saka ameiongoza England kutwaa nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia la FIFA baada ya kuichapa Ufaransa mabao 6-4.
Saka aling’ara kwa kufunga hat-trick, akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi na kuisaidia England kujinyakulia medali ya shaba baada ya mchezo wa kusisimua ulioshuhudia jumla ya mabao kumi. Ufaransa walimaliza mashindano katika nafasi ya nne.

Na katika soka la humu nchini, Mtwapa Premier League imeendelea kushika kasi kwa matokeo mbalimbali.
Mtwapa Senior iliichapa Posta Rangers mabao 3-1, huku Salim Mohammed, Karani Kombe na Walter Ocheka wakifunga mabao ya ushindi.
KP Laliga FC nayo iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Young Progressive, wakati Mtepeni FC ikiizidi nguvu Komboa FC kwa mabao 2-0.
Katika mechi nyingine, Kimbunga FC iliigaragaza Baraza FC mabao 3-0, huku Rophus Mlanda akifunga mawili. Nayo Mgandini FC iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Bomani FC.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Mtwapa Premier League Ali Nassir amezitaka timu zote kushikilia nidhamu ndani na nje ya uwanja, akisema ligi hiyo inalenga kukuza vipaji vya vijana na kuandaa wachezaji watakaoweza kucheza katika ligi za juu nchini na kimataifa.
